Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Isimani, William Lukuvi, umepokelewa na mamia ya wakazi wa Iringa na kupelekwa nyumbani kwake mtaa wa Gangilonga kwa ajili ya taratibu za mwisho.

Kwa mujibu wa ratiba, ibada na kuagwa kwa mwili huo kunatarajiwa kufanyika kesho, huku mazishi yakipangwa kufanyika Jumanne kwa utaratibu wa kichifu.

Mwandishi wetu, Muhammad Nyaulingo, amezungumza na mmoja wa wazee wa kimila ambaye ameeleza kuwa mazishi ya kichifu hufuata taratibu maalum za heshima, ikiwemo ibada za kimila na ushirikishwaji wa jamii katika kumzika kiongozi huyo kwa hadhi yake.

✍ Mohammad Nyaulingo
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *