Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewatoa wasiwasi wananchi kuhusiana na madai dhidi ya matumizi ya fedha za mikopo ya Serikali na kueleza kuwa ushahidi wa matumizi ya mikopo hiyo uko mbele ya macho yao kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa nchi nzima ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara ambazo huleta tija kwa wananchi kupitia shughuli za kiuchumi, biashara na huduma mbalimbali.

Waziri Ulega ametoa kauli hiyo wakati akikagua ujenzi wa barabara ya kilometa 160 kati ya Mnivata – Newala – Masasi inayojengwa kwa kiwango cha lami na kuongeza kuwa mikopo inayochukuliwa na Serikali inalenga kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi kupitia miradi ya maendeleo ambayo huwapa fursa wananchi kunufaika nayo kupitia shughuli zao za kila siku.��

Naye Mbunge wa Nanyamba, Abdallah Chikota amewahimiza wananchi hao kuonesha ushahidi wa barabara hiyo na kueleza umuhimu wake kwa maendeleo yao badala ya kukubali kupotoshwa na kauli zinazodai kuwa fedha za mikopo ya maendeleo hazijulikani zilikoelekezwa.

��Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *