#HABARI: Mrisho Hassan Nambwenya mwenye umri wa miaka 13 mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Mikindani, amefariki kwa kuzama Baharini na mwili wake kupatikana baada ya msako mkali wa saa kadhaa, huku watoto wenzake 2 wakinusurika baada ya kuokolewa.

Wakizungumzia tukio hilo kwenye Pwani ya Kijiji cha Mvita kulikotokea ajali hiyo, wamesema Mtumbwi huo ulikuwa ukiendeshwa na watoto hao huku Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mikindani Dkt. Mariam Mohamed akithibitisha kupokea mwili wa mtoto huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Operasheni wa Jeshi la Zima Moto na Uoakoaji mkoani Mtwara, ambapo lilishiriki kwenye msako wa mtoto huyo ASF Ambrose Ndunguru ametoa ushauri kwa wazazi na walezi.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
‎Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
‎Capitalradio Tanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *