
Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imetoa taarifa ikitangaza kuwa jeshi hilo limetekeleza awamu ya pili ya wimbi la 86 la Oparesheni Ahadi ya Kweli-4 dhidi ya kitongoji cha viwanda cha Neot Hovav huko Beersheba kusini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina (Israel).
Katika wimbi la 86 la Oparesheni ya Ahadi ya Kweli-4; Kikosi cha anga cha Jeshi la IRGC kimeshambulia kitongoji cha viwanda cha Neot Hovav huko Beersheba kusini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kwa mifumo ya makombora ya balistiki ikiwa ni katika kujibu vikali mashambulizi ya kinyama ya mhimili wa Marekani- Uzayuni dhidi ya maeneo ya viwanda ya Iran na katika kuendelea kutoa kipigo kwa sekta ya viwanda ya vibaraka wa Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
Umeme wa eneo hilo ulizima kikamilifu baada ya milipuko kadhaa mfululizo.
Aidha vituo vya kijeshi vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika jangwa la Negev, kamandi ya jeshi la utawala huo katika eneo la kaskazini na vituo vya usalama huko Quds inayokaliwa kwa mabavu na Tel Aviv vimeshambuliwa kwa makombora ya balistiki na droni za hujuma za Iran.