Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imetoa taarifa ikitangaza kuwa jeshi hilo limetekeleza marhala ya pili ya wimbi la 86 la Oparesheni Ahadi ya Kweli-4 dhidi ya kitongoji cha viwanda cha Neot Hovav huko Beersheba kusini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Katika kuendelea wimbi la 86 la Oparesheni ya Ahadi ya Kweli-4; Kikosi cha anga  cha Jeshi la IRGC likimeshambulia kitongoji cha viwanda cha Neot Hovav huko Beersheba kusini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kwa mifumo ya makombora ya balistiki ikiwa ni katika kujibu vikal mashambulizi ya kinyama ya mhimili wa Marekani- Uzayuni dhidi ya maeneo ya viwanda ya Iran na katika kuendelea kutoa kipigo kwa sekta ya viwanda ya vibaraka wa Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi. 

Eneo hilo lilizima lote baada ya kujiri milipuko ya mfululizo. 

Aidha vituo vya kijeshi vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika jangwa la Negev, kamandi ya jeshi la utawala huo katika eneo la kaskazini na vituo vya usalama huko Quds inayokaliwa kwa mabavu na Tel Aviv vimeshambuliwa kwa makombora ya balistiki na droni za hujuma za Iran. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *