Mazungumzo ya ngazi ya juu ya shirika la kimataifa la biashara, WTO, yamemalizika rasmi nchini Cameroon bila makubaliano yoyote muhimu ikiwemo kushindwa kuongeza muda wa kupiga marufuku ushuru wa forodha kwa biashara ya mtandaoni, baada ya kuwepo mgawanyiko.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa shirika hilo Ngozi Okonjjo Iweala amesema kwa siku nne za mazungumzo  ya kina ,WTO ilifanya kadri ya uwezo wake lakini ,makubaliano yalishindikana.

Maswala muhimu yaliyogeuka vizingiti ni pamoja na kurejea kwa maarufuku ya ushuru kwenye uchumi wa kidijiti na maswala ya kilimo.

Brazil katika dakika ya mwisho ilizuia rasimu kuhusu uchumi wa kidijiti ilipinga kutokuwa na maendeleo kwenye mazungumzo kuhusu kilimo.

Mawaziri wa biashara na wajumbe ,walipaswa kuja na mpango kazi wa kuchochea uwezo wa WTO ambao umeathirika kutokana na maswala tofauti ya kidunia ikiwemo namna Marekani imeendelea kutatiza biashara ya dunia kwa kutangaza ushuru wa bidhaa kutoka nje.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *