
Rais wa Marekani, Donald Trump, ametishia kuharibu kitovu cha usafirishaji wa mafuta ya Iran kwenye kisiwa cha Kharg, ikiwemo visima vyake na vinu vya nishati ikiwa nchi hiyo haitakubali mkataba wa kusitisha vita.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Truth Social, Trump aliandika kuwa huenda makubaliano na Iran yakafikiwa wiki hii na kwamba wanajadiliana na utawala ambao unaonesha kuwa tayari kufikia Suluhu, lakini bado akatoa onyo kwa Tehran.
Trump amedai kuwa hatua kubwa imepigwa, lakini ikiwa kwa sababu yoyote ile makubaliano hayatafikiwa na ikiwa mlango bahari wa Hormuzi hautafunguliwa kwa biashara, basi nchi yake itakamilisjha operesheni yake kwa kulipua na kuharibu kabisa kituo chake cha nishati, visima vya mafuta na kisiwa cha Khargi.
Siku ya Jumapili akizungumza akiwa ndani ya Air Force On, Trump alisema kuwa nchi yake na Israel wamefanikiwa kubadili utawala wa Iran kupitia vita waliyoanzisha mwezi mmoja uliopita, akisifu mauaji ya viongozi wa Tehran waliyoyafanya.
Hata hivyo onyo lake linakuja wakati ambapo tehran kwa upande wake, inasisitiza kuwa itajibu kwa kiwango kinachostahili mashambulio ya Marekani na Israel kulenga miundombinu yake muhimu.