
Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC, kuanzia leo inazindua zoezi endelevu la kujiadikisha kwa wapiga kura wapya wapatao zaidi ya Milioni 2.5 kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mwenyekiti wa Tume hiyo Erustus Ethekon, amesema zoezi hilo litafayika nchi nzima na wanaolengwa ni vijana ambao hawajawahi kupiga kura.
Katika mchakato huu, Tume hiyo inasema, zoezi hili linaondoka kwenye maeneo bunge kwenda mitaani na vijijini ili kuwapata wapiga kura wapya.
Aidha, vituo vya kujiandikisha pia vitakuwa katika vyuo vikuu na vile vya Kati ili kuwapaya vijana zaidi.
Hatua hii inakuja, wakati wanaharakati vijana nchini Kenya, maarufu kama Gen Z, wakianzisha vuguvugu wanaloliita Niko Kadi kuwahamasisha vijana kujitokeza na kujiandikisha kwa wingi kama wapiga kura.
Kenya itakuwa na uchaguzi mkuu mwezi Agosti mwaka ujao, ambapo watapiga kura kumchagua rais, Magavana, Maseneta, Wabunge na wawakilishi wa wanawake.