Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Marekani Donald Trump ameliambia gazeti la Financial Times
kwamba anaweza “kuchukua mafuta nchini Iran” na ikiwezekana akakiteka
Kisiwa cha Kharg ambacho ni kitovu kikuu cha mafuta nchini humo.
“Kusema ukweli, jambo ninalotaka zaidi ni
kuchukua mafuta nchini Iran lakini baadhi ya watu wajinga huko Marekani
wanasema: ‘Kwa nini unafanya hivyo?’ Lakini ni watu wajinga,” alisema.
Trump alipendekeza hatua hiyo inaweza kumaanisha
kuchukua kisiwa cha Kharg. “Pengine tuchukue Kisiwa cha Kharg, au tuachane
nacho. Tuna chaguzi nyingi,” Trump aliambia Financial Times. “Inamaanisha pia kuwa tulipaswa kuwa huko [katika Kisiwa cha Kharg] kwa
muda.”
Alipoulizwa kuhusu ulinzi wa Iran katika kisiwa
hicho alisema: “Sidhani kama wana utetezi wowote. Tunaweza kukichukua kwa
urahisi sana.”
Kauli hiyo ya rais inakuja huku wanajeshi 3,500
zaidi wa Marekani wakiwasili Mashariki ya Kati, hofu ya wanajeshi wa Marekani kijiunga
na mashambulizi ya Iran ikiongezeka.
Trump aliongeza kuwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa
moja kati ya Marekani na Iran kupitia “mabalozi” wa Pakistan yalikuwa
yanaendelea vizuri, lakini hakugusia suala makubaliano ya kusitisha mapigano
yanaweza kufikiwa hivi karibuni.
“Mkataba unaweza kufikiwa haraka,”
alisema.
Maelezo zaidi: