
Urusi hivi leo iliagiza kuondoka nchini humo kwa mwanadiplomasia mmoja wa Uingereza kwa madai ya kufanya kufanya ujasusi, tuhuma ambazo London imezipuuza na kuziita “ujinga”.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, shirika la ujasusi la Moscow, FSB, linadai mwanadiplomasia huyo alitoa taarifa za uongo wakati akiomba kibali kuingia nchini humo, na pia kujaribu kupata taarifa za siri wakati wa mikutano isiyo rasmi ya kiuchumi.
Mbali na kutakiwa kuondoka, stakabadhi za mwanadiplomasia huyo zimebatilishwa, hatua ambayo msemaji wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza ameitaja kuwa upuuzi mtupu na kuishutumu Urusi kwa kampeni ya uchokozi na iliyoratibiwa ya unyanyasaji dhidi ya wanadiplomasia wa London.
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Uingereza na Urusi umezidi kuwa mbaya katika miaka ya hivi karibuni, huku nchi zote mbili zikiwafukuza baadhi ya wanadiplomasia wao tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo 2022.