Mbio za Akili Alumni Marathon zitafanyika Aprili 06 mwaka huu kwenye viwanja vya Leaders Club Dar es salaam.
Maandalizi ya mbio hizo yameendelea kupamba moto ambapo washiriki mbalimbali wamejitokeza eneo la Mliman City kujisajili kwa ajili ya kujiandaa kwenye tukio hilo linalotarajiwa kuwakutanisha washiriki wa kila aina wadogo , wakubwa hadi wazee.
Baadhi ya wadau na washiriki waliojitokeza kufanya usajili wameeleza namna ambavyo mbio hizo zitakavyoongeza chachu ya maendeleo kwenye elimu na kuvumbua mafanikio makubwa ya vijana ndani na nje ya nchi.
Malengo yam bio hizo ni kukusanya zaidi ya dola za kimarekani milion 1.2 kwa ajili ya kuwadhamini wanafunzi 100 wa kitanzania.
Mgeni rasmi wa mbio hiyo ni Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, na kutakuwa nambio za aina tatu ambazo ni Km 5, Km 10 na Km 21.
(Feed generated with FetchRSS)