Mwaka huu kwenye michuano ya kombe la Dunia, Afrika itaweka historia kwa kuwa na timu 10, hatua kubwa katika maendeleo ya soka la Afrika.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Idadi hii ya timu 10 imekuja shukrani kwa uamuzi wa shirikisho la soka duniani kuamua kupanua wigo wa timu zitakazoshiriki kombe la dunia la mwaka huu kutoka 32 hadi 48.

Miongoni mwa timu zilizofuzu ni miamba ya soka ya Afrika Morocco, Tunisia, Misri, Algeria, Senegal, Ivory Coast na Ghana.

Nyingine ni Cape Verde, Afrika Kusini, na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

DRC na Iraq ndizo zilikuwa timu za mwisho kukamilisha orodha ya timu zilizofuzu kucheza fainali za mwaka huu, baada ya kupata ushindi dhidi ya Jamaica na Bolivia mtawalia.

Wawakilishi wa kwanza toka Afrika kutupa karata ya kwanza watakuwa ni Afrika Kusini watakaokuwa kundi A pamoja na wenyeji Mexico, Korea Kusini na Jamuhuri ya Cheki, na mechi ya kwanza ya Bafanabafana itakuwa dhidi ya Mexico Juni 11.

Morocco walio kundi C na Brazil, Scotland na Haiti, watachezaji Juni 14 dhidi ya Brazil, huku Juni 17 wawakilishi pekee toka ukanda wa Afrika Mashariki DRC walio kwenye kundi K, pamoja na Ureno, Colombia na Uzbekistan, watafungua pazia na Ureno.

Makundi mengine ni pamoja na Ivory Coast iliyo kwenye kundi E pamoja na Ujerumani, Ecuador na Curacao, tembo wa Ivory coast wakitarajiwa kutupa karata ya kwanza Juni 15 dhidi ya Ecuador. Tunisia wao wako kwenye kundi F na Uholanzi, Japan na Uswidi na watacheza mechi yao ya kwanza Juni 15 dhidi Uswidi.

Misri wao wako kwenye kundi G na Ubelgiji, Iran na New Zealand, na mechi yao ya kwanza itakuwa Juni 15 dhidi ya Ubelgiji. Cape Verde wao wako kundi H sambamba na Uhispania, Uruguay na Saudi Arabia na mechi ya Kwanza watacheza Juni 15 dhidi ya Uhispania.

Senegal wao watakuwa kundi I na Ufaransa, Norway na Iraq na mechi ya Kwanza watacheza Juni 16 dhidi ya Ufaransa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *