
WAWEKEZAJI na wazalishaji nchini wametakiwa kutumia huduma za Shirika la Viwango Tanzania (TBS), hususan katika sekta ya vipimo, ili kuimarisha ubora wa bidhaa zinazozalishwa nchini. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Metrolojia wa TBS, Joseph Kadenge amesema metrolojia ni msingi muhimu wa ubora, unaohakikisha usahihi wa vipimo katika mashine za uzalishaji.
Ameeleza kuwa ubora wa bidhaa hutegemea usahihi wa mashine, hivyo vipimo visipokuwa sahihi huathiri ubora wa bidhaa. Kadenge ameongeza kuwa TBS ina Maabara ya Taifa ya Vipimo (National Metrology Laboratory) iliyotambuliwa kimataifa kupitia BIPM, pamoja na kupata ithibati ya umahiri kutoka SADCAS.
Amesema huduma za ugezi zinapatikana kwa viwango vya kimataifa, na kuwahimiza wawekezaji kuendelea kuwekeza nchini bila hofu. SOMA: TBS yanogesha mambo ujenzi maabara Dodoma, Mwanza