DAR ES SALAAM: MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Amina  Said amewataka wanawake wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Mabibo kushikamana kwani wanawake ni kioo kwa jamii na wanamchango mkubwa kwa taifa na jamii kwa ujumla .

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kata ya mabibo na kusema kuwa atawapatia wanawake hao vifss mtaji huku akitaka wavitumie vyema ili viweze kuwanufaisha kujikwamua kiichumi.

Aidha Amina amesema mafunzo waliyoyapata wanawake hao katika kongomano hilo wayafanyie kazi ikiwemo malezi ya watoto kwani dunia ya sasa imebadilika.

Naye, Shani Swago Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania ( UWT) Kata ya Mabibo amesema lengo la kongamano ni kujenga jamii imara na yenye mshikamano na wanajadili masuala yanayoihusu jamii ikiwemo na uchumi wa kifedha.

Aidha Shani amesema jamii inapaswa kukemea ukatili wa kijinsia unaofanyika kwa jamii na elimu ni muhimu kutolewa kwa jamii husika ili wanaofanya mambo hayo waweze kubainika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *