Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu, Aprili 6, Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuiangamiza Iran Jumanne jioni ikiwa Tehran haitajibu uamuzi wake kwa kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz, muhimu kwa usambazaji wa mafuta duniani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Nchi nzima inaweza kuharibiwa katika usiku mmoja,” ambao unaweza kuwa Jumanne usiku, rais wa Marekani ametangaza. Wakati huo huo jeshi la Iran limelaani “maneno ya kiburi,” likisema kupitia msemaji wake kwamba taarifa kama hizo “hazina athari” kwenye operesheni zake.

Wakati wa mkutano huo huo na waandishi wa habari, Donald Trump pia ametoa maelezo kuhusu operesheni ya uokoaji kwa wanajeshi wawili wa anga wa Marekani waliookolewa nchini Iran katika siku za hivi karibuni. 

Misheni ya kwanza ya uokoaji ilihusisha ndege “21”, amesema, huku ya pili ikihusisha “ndege 155… Tuliwarejesha wotenyumbani ardhi ya Iran.” Pia alibainisha kuwa ndege mbili za usafiri wa kijeshi zilikwama kwenye mchanga na ilibidi ziharibiwe.

Hayo yanajiri wakati jeshi la Israel, siku ya Jumatatu usiku, lilitangaza “wimbi” la mashambulizi ya anga dhidi ya Iran na pia liliripoti kugundua makombora ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *