
Zeine Ould Zeidane wa Mauritania atachukua nafasi ya mkuu Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kaika kanda ya Afrika mnamo Mei 1, 2026. Atachukua nafasi ya Abebe Aemro Selassie, ambaye ameshikilia wadhifa huo tangu mwaka 2016. “Nina uhakika kwamba ataongoza IMF katika kanda ya Afrika kwa mafanikio na kwa imani,” amesema Mkurugenzi Mkuu wa IMF Kristalina Georgieva.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Zeine Ould Zeidane alijiunga na IMF mnamo mwaka 2012. Alihudumu kama Naibu Mkurugenzi wa IMF katika kanda za Mashariki ya Kati na Asia ya Kati, ambapo alisimamia uhusiano na nchi za Ghuba. Katika jukumu hili la kimkakati, raia huyo wa Mauritania alisaidia sana kufungua ofisi ya kikanda huko Riyadh, nchini Saudi Arabia.
Kwa hivyo ni kiongozi wa IMF mwenye uzoefu. Kabla ya kuchukua wadhifa wake Mashariki ya Kati, Zeine Ould Zeidane alikuwa naibu mkurugenzi wa kitengo cha kifedha cha IMF katika kanda ya Afrika. Ndani ya taasisi hiyo, mkuu mpya wa IMF katika kanda ya Afrika anaelezewa kuwa na “ujuzi bora wa mahusiano ya watu” na “mtandao tajiri wa mawasiliano kote barani.” Kristalina Georgieva, Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, alibainisha “utulivu” wake na “ustadi wake wa kufikiri,” ambao “ulionekana kuwa na ufanisi hasa katika kutatua matatizo magumu na nyeti.”
Katika taasisi hiyo, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 60 aliongoza kazi inayohusiana na sera ya utawala. Wakati wa mlipuko wa UViko-19, alifanya kazi ili kushughulikia vyema mahitaji ya bara hilo, kwani nchi nyingi zilikabiliwa na changamoto ya deni. Kabla ya kujiunga na IMF, mchumi huyu, ambaye ana shahada ya udaktari katika hisabati inayotumika na shahada ya Uzamili katika uchumi mkuu kutoka Chuo Kikuu cha Nice, Ufaransa, alishikilia nafasi za juu nchini Mauritania.
Mshauri wa wa rais Maaouiya Ould Sid’Ahmed Taya katika masuala ya masuala ya uchumi na gavana wa benki kuu ya Mauritania, Zeine Ould Zeidane aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu mnamo mwaka 2007 na rais Sidi Mohamed Ould Cheikh Abdallahi. Wakati wa mwaka wake wa kwanza akihudumu kama waziri mkuu, alijitofautisha kupitia hatua za kubana matumizi zilizotekelezwa ili kuleta utulivu wa fedha za nchi.