
Ingawa uhusiano kati ya majirani hao wawili umekuwa mgumu tangu mapinduzi dhidi ya Rais Mohamed Bazoum huko Niamey mnamo mwezi Julai 2023, kuwasili kwa rais mpya nchini Benin kunaweza kubadilisha hali hiyo. Huko Cotonou, raia wanasubiri kwa hamu kufunguliwa tena kwa mpaka kati ya nchi hizo mbili, ambao bado umefungwa hadi leo.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu maalum huko Cotonou, Magali Lagrange
Wakati wapiga kura wa Benin wakielekea kwenye vituo vya kupigia kura siku ya Jumapili, Aprili 12, kuchagua kati ya Romuald Wadagni, mgombea wa kambi ya rais, na Paul Hounkpè, mgombea wa FCBE – chama cha upinzani- ambaye atamrithi Rais Patrice Talon, je, kuwasili kwa kiongozi mpya kunaweza kubadilisha uhusiano ambao bado ni mgumu kati ya Benin na jirani yake Niger, hali ambayo imeendelea tangu mapinduzi huko Niamey mnamo mwezi Julai 2023?
Nchini humo, matarajio ni makubwa katika hatua hii, kama ilivyoelezwa na Abdou, raia wa Niger, ambaye ameishi Cotonou kwa takriban miaka kumi na tano. Ingawa hakika anahisi yuko nyumbani katika mji mkuu wa kiuchumi wa Benin – “Hakuna ubaguzi wa rangi, hakuna maneneo yanayomtenga kama ‘Yeye ni Mniger, hatuelewani naye, tutamtendea vibaya,’ hapana,” anabainisha – hali yake haimzuii kutumaini kurekebishwa kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili: “Tunatarajia mengi kutoka kwa rais mpya. Kuna haja ya kuwa na mazungumzo na Niger ili kila mtu aweze kuwa na furaha. Miaka mitatu ya kutoelewana ni mingi sana!” pia amesema.
Romuald Wadagni: “Tunapaswa kuzungumza, hatuna chaguo
” Miongoni mwa maamuzi yanayotarajiwa zaidi katika hali kama hiyo: kufunguliwa tena kwa mpaka kati ya nchi hizo mbili, ambao bado umefungwa miaka mitatu baada ya mapinduzi huko Niamey. Kwa sababu wakati wa kusafiri kwa basi kati ya Cotonou na Niamey bado inawezekana leo, safari ni ngumu zaidi, ikiwa na muda mrefu wa kusafiri na gharama kubwa zaidi. “Kusafirisha abiria ni ngumu sana kwa kuvuka Mto [Niger]. Kwa mfano, ikiwa una mizigo, lazima ulipie baiskeli ya magurudumu matatu unapofika Malanville [mji wa Benin uliopo kwenye mpaka na Niger]. Kwa hivyo, ili kusafiri hadi Niamey, unahitaji kuwa na pesa nyingi. Kidogo tu hakitoshi,” anaelezea Fulbert Anani, ambaye anafanya kazi katika kampuni ya Niger STM huko Cotonou.
“Tunapaswa kuzungumza, hatuna chaguo,” amesema Romuald Wadagni, mgombea urais, hivi karibuni, akiongeza: “Tutachukua fursa hiyo kuwafikia majirani zetu ambao wanajitahidi kutuamini.”