Tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu usitishaji wa mapigano kwa wiki mbili na Iran, sasa linatoa nafasi ya kujadiliana kuhusu agenda 10 zilizopendekezwa na Tehran kumaliza vita. Nini kipo kwenye mapendekezo hayo?
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Baada ya siku 39 za mapigano mashariki ya kati, Iran na Marekani zimekubaliana kusitisha mapigano kwa kipindi cha wiki mbili.
Rais wa Marekani Donald Trump amekubali nchi yake kutoishambulia Iran kwa kipindi cha wiki mbili.
Iran kwa upande imekubali kuufungua mlango wa bahari wa Hormuz.
Kipindi cha wiki mbili cha usitishaji wa mapigano kinatoa nafasi kwa Marekani na Iran kukutana kwa mazungumzo nchini Pakistan Ijumaa ya wiki hii.
Iran ilikuwa imependekeza agenda 10 kwa Marekani ambazo kwa mujibu wa Rais Trump zinatoa nafasi ya kujadiliwa zaidi.
Iran inataka wanajeshi wa Marekani kuondolewa katika eneo la Mashariki ya kati.
Tehran aidha inataka kuwepo kwa kanuni zinazowesha safari za meli katika Mlango wa bahari wa Hormuz kwa uangalizi wa Iran.
Aidha inataka vita kumalizika dhidi ya makundi yenye silaha yanayoiunga mkono Iran.
Iran inataka kufidiwa uharibifu wote uliotokana na mashambulio ya Marekani.
Iran pia inataka mali zake zilizozuiwa kuachiwa pamoja na kuondolewa vikwazo vyote dhidi yake.
Rais Trump anasema kipindi cha usitishaji wa mapigano kitatoa nafasi ya kujadiliwa zaidi kwa mapendekezo hayo na kuja na rasimu ya mwisho.