Borussia Dortmund wanafikiria kufanya jaribio la tatu kumsajili winga wa England, Jadon Sancho (26), ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo huko Aston Villa na anatarajiwa kuondoka Manchester United kama mchezaji huru

Safari ya Jadon Sancho katika klabu ya Borussia Dortmund ilianza mwaka 2017 alipohama kutoka akademi ya Manchester City akiwa na umri wa miaka 17. Dortmund walimpa nafasi mapema, na taratibu alianza kuonyesha kipaji chake cha kasi, chenga na ubunifu uwanjani.

Katika misimu iliyofuata, hasa 2018/19 na 2019/20 ndani ya ligi ya Bundesliga, Sancho aling’ara sana kwa kufunga mabao na kutoa assists nyingi. Alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Dortmund na akawa miongoni mwa vijana bora zaidi barani Ulaya. Mwaka 2021 aliisaidia timu kushinda DFB-Pokal kabla ya kuhamia Manchester United.

Baada ya kipindi kigumu England, mwaka 2024 Sancho alirejea tena kwa mkopo katika klabu ya Borussia Dortmund. Kurudi kwake kulimsaidia kurejesha kiwango na kujiamini, na mashabiki walimkaribisha tena kama nyota wao wa zamani.

#starTvupdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *