Makali ya kupanda kwa bei ya mafuta nchini yameanza kuumiza wananchi katika maeneo mbalimbali, ambapo wafanyabiashara katika soko kuu la Wilaya ya Newala wamelalamikia ongezeko la bei za baadhi ya bidhaa, ikiwemo mafuta ya kula ambayo yamepanda kutoka shilingi 45,000 hadi 57,000 kwa lita 10, pamoja na vilainishi vya mitambo na vipuri vya magari.

Wakati huo huo, nauli za bodaboda wa eneo hilo zimeongezeka mara mbili ya kiwango cha awali.

Nini kifanyike kukabiliana na ongezeko la bei za bidhaa na nauli nchini? Tuandikie maoni yako na tutayasoma #AdhuhuriLive saa 7:00 #UTV

#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *