Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo, Aprili 10, 2026 kimekuta na kufanya mazungumzo na Rais mstaafu wa Malawi, Dkt Lazarus Chakwera

Jopo hilo la viongozi Chadema limeongozwa na Makamu Mwenyekiti, John Heche.

Rais mstaafu Chakwera anaongoza ujumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola ambao wapo nchini kwa ajili ya kufuatilia matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyoripotiwa kutokea Oktoba 29 ambako wananchi wengi walipoteza maisha.

Viongozi wengine wa Chadema ni Katibu Mkuu John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Bara,Manigolugwa, Mwanasheria Mkuu wa Chama, Rugemeleza Nshala, Mwenyekiti wa Bazecha Taifa Susan Lyimo na rafiki wa Chadema, Jeenerali Twaha Ulimwengu

Katika kikao hicho, Dkt Chakwera amepokea taarifa ya msimamo wa Kamati Kuu ya Chadema. Aidha, amepewa maelezo kuhusu matukio yaliyotokea kabla na baada ya Oktoba 29, ikiwamo kukamatwa kwa Mwenyekiti wa chama, Tundu Lissu, pamoja na matukio ya utekaji

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *