
Nchini Kenya, utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa idadi kubwa ya raia wa taifa hilo wanaendelea kuvutiwa kufanya kazi katika nchi za Ghuba, licha ya kuongezeka kwa ripoti za ukiukaji wa haki za binadamu katika miaka ya karibuni.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ripoti hiyo iliyochapishwa kwenye mtandao wa The Conversation inaonyesha kuwa kufikia mwaka 2025, takribani Wakenya laki 3 walikuwa wakifanya kazi katika nchi za Saudi Arabia, Qatar na Falme za kiarabu.
Aidha, fedha zinazotumwa nyumbani kutoka mataifa hayo zilifikia dola milioni 40 mwaka jana, ingawa mwaka huu hali hiyo huenda ikaathiriwa na mvutano wa kisiasa na vita vinavyoendelea kati ya Marekani, Israel na Iran.
Hata hivyo, baadhi ya wafanyakazi wanakiri kuwepo kwa changamoto kama vile unyanyasaji wa kingono, mateso, kufanya kazi bila mapumziko, na ukiukaji wa mikataba ya ajira huku wengine wakiripoti kupokea vitisho kutoka kwa waajiri wao.
Licha ya juhudi za kidiplomasia kati ya Kenya na mataifa hayo, vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vinaendelea kuripotiwa.