Donald Trump amemkosoa vikali Papa Leo XIV kwenye mitandao ya kijamii
baada ya kiongozi wa kwanza wa Marekani wa Kanisa Katoliki Duniani kulaani
tishio la rais wa Marekani dhidi ya Iran.

Katika chapisho refu kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social,
rais huyo wa Marekani aliandi Papa “ni mbaya kwa Sera ya Kigeni”.

“Simtaki Papa ambaye anadhani ni sawa kwa Iran kuwa na Silaha ya
Nyuklia,” Trump alisema.

Akiorodhesha malalamiko mengine dhidi ya Papa, Trump aliandika kwamba
Papa Leo ni “Weak on Crime, Weak on Nuclear Weapons”.

Wiki iliyopita, Papa Leo alikosoa tishio la Trump kwamba “ataiangamiza
Iran usiku wa leo” nchi hiyo isipofikia makubaliano ya kumaliza vita.

Akisisitiza kuwa tamko kama hilo “halikubaliki”, Papa aliongeza
kusema: “Kuna maswali ya sheria ya kimataifa, lakini zaidi ya yote, ni suala
la kimaadili.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *