Wananchi 1,730 wanaopisha njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 220 kutoka Masasi hadi Mahumbika wanatarajiwa kupewa fidia ya Shilingi Bilioni 5.1 ambazo Serikali imezitenga katika mwaka wa fedha wa 2025/2026.

Taarifa hiyo imetolewa mapema leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba alipokuwa akitoa majibu kwa swali la Mbunge wa Ndanda, Faraji Buriani Nandala.

Wananchi hao 1,730 wanatoka katika kata za Chikukwe, Chigugu, Chigundi, Mwena, Ndanda na Nanganga.

Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *