YANGA SC vs MBEYA CITY: “Tunategemea mchezo mgumu kesho, mgumu kwa kiwango kikubwa…”-Kocha wa Yanga SC, Pedro Goncalves amesema wanatarajia mchezo mgumu kesho Aprili 16, 2026 kutoka kwa wapinzani wao Mbeya City, kwenye mchezo wao wa NBC Premier League, kutokana na ubora wa timu hiyo kwa sasa.
Pedro amesema kikosi cha Yanga kimejiandaa vema na lengo kuu la timu kwenye mchezo huo ni kupata alama tatu.
Kwa upande wa mchezji wa timu hiyo Israel Mwenda amesema wanatambua ugumu utakaokuwepo kwenye mchezo huo ila watajituma zaidi ili kupata matokeo na kuepuka kutoka katika mbio za ubingwa msimu huu.
Mwandishi Katherini Shirima
Mhariri:@allymufti_tz
#NBCPL #YangaSC #MbeyaCity #YangaSCMbeyaCityFC
(Feed generated with FetchRSS)