Kufuatia wilaya ya Kongwa kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya ngazi mbalimbali za elimu kwa mwaka 2025, walimu wanaofundisha kwenye wilaya hiyo wamepongezwa ikiwa ni sehemu ya hamasa ya kuendeleza mafanikio hayo.

Sambamba na pongezi hizo walimu hao wameiomba serikali ya wilaya hiyo kurejesha posho ya ufundishaji kwa walimu waliyodai imekuwa chachu ya mafanikio hayo ambapo mwakilishi wa walimu vijana mkoa wa Dodoma kutoka CWT, Issa Mfwango amesema licha ya mchango mkubwa wanaoutoa, bado walimu wanakosa posho au bonasi yoyote hata wanapofanya katika muda wa ziada.

Taarifa ya Henry Masanja.

Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *