Wiki saba zilizopita, Marekani na Israel zilitekeleza mashambulizi dhidi ya Iran. Vita hivi vilienea haraka katika eneo lote. Lakini katika saa chache tu siku ya Ijumaa Aprili 17, hali katika Mashariki ya Kati ilibadilika sana kutokana na utekelezaji wa kusitisha mapigano nchini Lebanon na kutangazwa kwa kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz. Kuhusu mashambulizi ya angani ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, yalikuwa tayari yamemalizika kwa makubaliano ya usitishaji mapigano Aprili 8.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ingawa bado ni mapema sana kutangaza kumaliziika kwa vita hivi, ni hali gani inayojitokeza katika eneo hilo baada ya matukio haya yasiyo ya kawaida? Ikishambuliwa kwa nguvu kamili ya majeshi ya Marekani na Israel, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijaanguka. Inadai ushindi lakini sasa lazima ikabiliane na ugumu wa kiuchumi usio wa kawaida, na hakuna uhakika kwamba utawala huo umerejesha uhalali wake kwa raia, walionyamazishwa na ukandamizaji.

Kwa mataifa ya Ghuba ya Kiarabu, vita hivi vimeonyesha kwamba muungano wao na Washington una mipaka yake. Makombora na ndege zisizo na rubani za Iran zilidondoshwa katika nchi hizi zinazozalisha mafuta, zikiwa na hasira baada ya kugundua kwamba Donald Trump hakuwajali sana na anapendelea kufuata msimamo wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Nchini Israel, vita hivi vinaonekana kama mwendelezo wa vile vilivyoanzishwa baada ya Oktoba 7, 2023, huku nia ya Israel ikitajwa kuwa ni kuunda upya Mashariki ya Kati kwa nguvu zote.

Hata hivyo, mapigano yamekoma katika siku za hivi karibuni, na kuna imani inayoongezeka katika mazungumzo kati ya Iran na Marekani, na kati ya Israel na Lebanon. Lakini ni aina gani ya mazungumzo na matokeo gani yanaweza kutarajiwa baada ya kuzuka kwa vurugu ambazo Mashariki ya Kati imeshuhudia hivi punde?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *