
Wakati Iran ilipotangaza kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz, zaidi ya nchi arobaini zimekutana siku ya Ijumaa, Aprili 17, kujadili mustakabali wa ukanda huu wa baharini, ambao vizuizi vyake vina athari kubwa kwa uchumi wa dunia. Katikati ya majadiliano, kwa mpango wa Ufaransa na Uingereza, ilikuwa ni kulinda eneo hilo ili kusaidia meli za biashara zinazosafiri katika Ghuba.
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Emmanuel Macron na Keir Starmer walishangazwa Aprili 17: wakati viongozi wa Ufaransa na Uingereza walikuwa wakikutana na nchi zaidi ya arobaini kuamua kuanzisha mpango wa kulinda Mlango-Bahari wa Hormuz, walishangazwa na ujumbe wa Twitter kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi. “Kulingana na usitishaji mapigano nchini Lebanon, Mlango-Bahari wa Hormuz uko wazi kwa meli za biashara kwa muda unaosalia wa usitishaji mapigano,” aliandika.
“Hii yote ni hatua katika mwelekeo sahihi,” rais wa Ufaransa alijibu mara moja, huku akielezea kusikitishwa kuhusu masharti yaliyowekwa na Tehran, pamoja na kuendelea kuzuiwa kwa mlango bahari huo na jeshi la Marekani. Mwanzoni mwa mwezi Machi, Emmanuel Macron alipendekeza ujumbe wa kusimamia kufunguliwa tena kwa njia hii ya majini inayotenganisha Iran na mataifa ya Ghuba, mara tu mapigano yatakapokoma. Kwa hivyo, uamuzi wa Iran ulichukuliwa kwa wakati unaofaa, na “mpango ambao sote tumeufanya pamoja leo ni halali zaidi, kwa sababu utaimarisha matangazo haya kwa muda mfupi, na zaidi ya yote, kuyapa uwezekano wa kuendelea kudumu.”
Paris na London zinaongoza juhudi hizo, kama zilivyofanya mnamo mwezi Machi mwaka huu kwa muungano wa nchi zilizojitolea kwa ajili ya Ukraine. Mara tu mgogoro kati ya Iran na Marekani utakapomalizika kabisa, ujumbe wa kimataifa, “usioegemea upande wowote na huru, tofauti kabisa na pande zinazopigana,” unaweza kuulinda mlangobahari huo kwa meli za biashara zinazosafiri kupitia Ghuba. Mbali na nchi za Ulaya, Rais wa Korea Kusini Lee Jae-myung alishiriki katika mkutano huu, kama vile maataifa mengine ya Asia, kama vile China na Japan, na mataifa ya Mashariki ya Kati, ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia na Qatar, lakini katika ngazi ya mawaziri au wajumbe wengine wa serikali.
Nchi zaidi ya kumi, labda zaidi ya arobaini kushiriki
Hadi sasa, takriban nchi kumi zimethibitisha ushiriki wao. Kwa jumla, karibu arobaini zinaweza kushiriki. Pamoja na Emmanuel Macron na Keir Starmer, Giorgia Meloni, Waziri Mkuu wa Italia, bado hajazungumza. Kwa upande wake, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amejitofautisha kwa kuelezea nia yake ya ushiriki wa Marekani. Hili ni chaguo ambalo Emmanuel Macron hangefikiria, kwani hataki kuhusisha mhusika yeyote katika mzozo katika misheni hiyo.
“Ushiriki kama huo unaweza kujumuisha uondoaji wa mabomu na upelelezi wa baharini. Tunaweza kufanya hivyo,” Kansela wa Ujerumani alielezea. “Kwa hivyo, tutashiriki katika majadiliano zaidi kuhusu mipango ya kijeshi,” aliongeza. Waziri Mkuu wa Uingereza alisema mkutano mpya utafanyika wiki ijayo jijini London ili kufafanua kuhusu mipango hii ya kijeshi.
“Mpango huo hauna mana”
“Kwa kweli, mpango kama huo hauna maana,” alitangaza afisa wa zamani wa Ufaransa Guillaume Ancel. Makubaliano ya Marekani na Iran, ingawa si kamili, yangemaanisha kufunguliwa tena kwa safari za baharini katika Mlango-Bahari wa Hormuz. “
Donald Trump, kwa upande wake, ametoa mfululizo wa kauli zinazopingana kwenye mtandao wake wa Truth Social. Ingawa alikaribisha kufunguliwa tena kwa Mlango wa Hormuz, hata akiishukuru Iran, pia alithibitisha kujitolea kwake kudumisha kizuizi cha kijeshi. Na, bila kutaja mpango huo, alijibu: “Sasa kwa kuwa mgogoro wa Mlango wa Hormuz umekwisha, nilipokea simu kutoka NATO ikiuliza ikiwa tunahitaji msaada. Niliwaambia waendelee kubaki kando na suala hili, isipokuwa kama wanataka tu kujaza meli zao mafuta. Walioneka hawana msaada wowote wakati tulipouhitaji, ni kauli ya kusikitisha!
Kwa kweli, mpango huu wa Ufaransa na Uingereza—unaohusisha nchi zaidi ya thelathini—kuhakikisha Mlango-Bahari wa Hormuz mara vita vitakapomalizika hauna maana. Lengo lake pekee ni kutangaza kwamba hatutakubali kubaki chini ya udhibiti wa Iran au Marekani, ambayo ingeutumia kama njia ya kujipatia kipato katika aina ya mapambano ya kudumu.