
Vita nchini Sudan vilipoingia mwaka wake wa nne Aprili 15, 2026, wakimbizi wa Sudan waliokimbilia nchi jirani wanakabiliwa na matatizo makubwa. Matatizo haya yanazidishwa na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa misaada ya kigeni kutoka Marekani mwanzoni mwa mwaka 2025.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu maalum kutoka Gorom, Florence Miettaux
Kati ya Wasudan milioni 4.5 waliokimbia na kuvuka mipaka ya Sudan, 439,366 wametafuta hifadhi Sudan Kusini, kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR). Mojawapo ya kambi zinazowahifadhi ni Gorom, karibu na Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini. Zaidi ya wakimbizi 20,000 wa Sudan wanaishi katika kambi hyo, katika hali mbaya zaidi.
Wanawake zaidi ya hamsini wamekaa chini ya mti, kwenye ardhi tupu, kwenye mlango wa kambi ya Gorom nchini Sudan Kusini. Wanasubiri mgawanyo wa pesa taslimu wa kila mwezi, karibu dola10 kwa kila mtu. Wanufaika wa msaada huu sasa wamechaguliwa kwa uangalifu, kwani fedha ni chache sana, anaelezea Maker Deng, mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) huko Gorom.
“Tunakabiliwa na matatizo karibu kila siku, lakini hatuwezi kufanya chochote kwa sababu ya kupunguzwa kwa bajeti. Tunapunguza usaidizi wetu kwa walio katika mazingira magumu zaidi.”
Tangu kupunguzwa kwa ufadhili wa kibinadamu mapema mwaka wa 2025, huduma zote za kambi zimezorota. Hapo awali iliundwa kwa ajili ya wanafunzi 400, shule iliyoko katika kambi hiyo sasa ina wanafunzi 4,000, na hakuna pesa za kutosha kuwalipa walimu wa kutosha. Huduma ya afya ni sekta nyingine iliyoharibiwa, kulingana na Maker Deng.
“Wakimbizi wanafariki katika kituo cha afya cha Gorom kwa sababu hatuwezi kuwahamisha hadi Hospitali ya chuo kikuu cha Juba. Madaktari waliokuwa wakifanya kazi hapa Gorom wameondoka kwa sababu mishahara sasa ni midogo sana. Huduma ya kabla ya kujifungua haitolewi tena, na uzazi ambao ulikuwa ukifanyika hapa hauwezekani tena kwa sababu hakuna wakunga. Kupunguzwa kwa bajeti kumekuwa na athari mbaya kwa wakimbizi.”
Kulingana na afisa huyo, ufadhili wa kujitegemea kiuchumi kwa wakimbizi, kama vile mikopo midogo na programu za mafunzo, umesitishwa kabisa. Hii inawasukuma baadhi ya wakazi wa Gorom kujitosa katika migodi ya dhahabu ya mfumo wa kienyeji kusini mwa Juba, maeneo ambayo usalama wao unaweza kuhatarishwa wakati wowote.