Wakati maandalizi ya mkutano mkuu wa ALAT yakiendelea jijini Arusha, ambao pia utatumika kuwachagua viongozi wapya, baadhi ya wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wamezungumzia umuhimu wa chombo hicho pamoja na nafasi yake katika kuiwezesha serikali kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi.
Miongoni mwa wagombea hao ni Dkt. Nicas Mawazo Ginhu, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha, ambaye amesema ALAT ina jukumu kubwa la kusimamia maslahi ya serikali za mitaa pamoja na kuhakikisha kunakuwa na ushirikiano mzuri kati ya viongozi na wananchi.
“ALAT ni kiungo muhimu kati ya serikali kuu na serikali za mitaa. Kupitia jukwaa hili, tunaweza kuibua changamoto za wananchi na kuzifikisha katika mamlaka husika ili zipatiwe ufumbuzi wa haraka na wenye tija.”
Aidha, wagombea hao wameahidi kuimarisha uwajibikaji, uwazi pamoja na kushirikisha wadau wote katika kufanya maamuzi yatakayochochea maendeleo ya wananchi.
Mkutano mkuu wa ALAT unatarajiwa kufanyika katika siku chache zijazo hapa jijini Arusha, ukiwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuchagua viongozi watakaoongoza chombo hicho kwa kipindi kijacho.
(Feed generated with FetchRSS)