Mkurugenzi wa Idara ya Miliki wa Wakala wa Majengo Tanzania, TBA, FRV Said Mndeme amefanya ziara ya ukaguzi wilayani Chato mkoani Geita, kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya wakala huo pamoja na miradi ya maendeleo.

Katika ziara hiyo, ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato, ambapo amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa baada ya awamu ya kwanza ya ujenzi kukamilika na huduma za matibabu kuanza kutolewa kwa wananchi.

Katika awamu ya pili, TBA inaendelea na ujenzi wa miundombinu ikiwemo wodi yenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa 210, ambayo ipo katika hatua za mwisho kukamilika.

Aidha, Mndeme ametembelea pia jengo la huduma za mionzi, linalotarajiwa kuongeza ubora wa huduma za uchunguzi na matibabu.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *