Bei ya mafuta imepanda duniani baada ya maafisa wa Iran kusisitiza kuwa Lango Bahari la Hormuz katu halitarejea katika hali yake ya awali kwa manufaa ya Marekani na washirika wake.

Kigezo cha kimataifa cha mafuta ghafi aina ya Brent kilipanda kwa takribani asilimia 2.14 na kufikia dola 107.58 kwa pipa, huku mafuta ghafi ya Marekani yakiongezeka kwa asilimia 2.08 hadi dola 96.36 siku ya Jumapili.

Ongezeko hilo linafuatia onyo la Iran kwamba suala la Lango Bahari la Hormuz ni sehemu ya mamlaka yake ya kitaifa na halitarejea katika hali iliyokuwapo kabla ya vita vya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya nchi hii.

Katika mazungumzo ya simu siku ya Jumamosi, Rais wa Iran Masoud Pezeshkian alimweleza Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif kuwa hatua zinazoendelea za Marekani zinadhoofisha uaminifu na kufanya njia za mazungumzo kuwa ngumu zaidi.

Rais Pezeshkian pia alisisitiza kuwa Tehran haitaingia katika “mazungumzo ya kulazimishwa” na Marekani, na kwamba mzingiro wa baharini wa Marekani dhidi ya bandari za Iran lazima ukome kabla ya kufikiwa kwa makubaliano yoyote.

Uchokozi wa pamoja wa Marekani na Israel, pamoja na vitisho vya Marekani vya kuanzisha tena mashambulizi ya anga dhidi ya Iraniwapo hakutakuwa na makubaliano, sambamba na vizuizi vya usafirishaji kupitia Lango Bahari Hormuz, ni mambo ambayo yamepelekea bei ya mafuta katika masoko ya dunia.

Nchi za Afrika ni zimeathiriwa vibaya na vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran na ongezeko hilo la mafuta linatarajiwa kufanya hali iwe ngumu zaidi katika siku za usoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *