Katika kipindi ambacho dunia inaangalia mwenendo wa usalama na utulivu wa mataifa, kauli ya Serikali imeendelea kuweka msisitizo mkubwa juu ya jukumu lake la msingi la kulinda maisha na mali za wananchi.

Hili limebainishwa wazi na Mshauri wa Rais wa Diplomasia, Balozi Lazaro Nyalandu, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari vya kimataifa.

Akiweka msimamo wa serikali , Balozi Nyalandu amesema kuwa kauli ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaakisi dhamira ya dhati ya kuhakikisha kila mwananchi anaishi salama na kulindwa bila kujali changamoto zinazojitokeza.

Ripoti ya Tume ya Jaji Chande imekuwa nyenzo muhimu katika kuweka wazi ukweli ambao kwa muda ulikuwa ukizua maswali miongoni mwa wananchi, Kupitia uchunguzi wa kina, tume hiyo imeweka hadharani mambo muhimu, ikiwemo hatua zilizochukuliwa na serikali katika kukabiliana na hali hiyo, Hii ni ishara ya uwajibikaji na uwazi unaopaswa kupongezwa.

Kwa Muktadha huo ,Balozi Nyalandu amesema ni muhimu kutambua kuwa Ulinzi wa taifa si jukumu la serikali pekee, bali ni wajibu wa kila mmoja kushirikiana, ili kujenga jamii yenye amani, mshikamano, na maendeleo endelevu.

Msisitizo wab Balozi Nyalandu ni wakati wa kusimama pamoja, kuilinda nchi na kuhakikisha kuwa mustakabali wa vizazi vijavyo unabaki salama na thabiti.

#starTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *