Bohari ya Dawa (MSD), imepata mafanikio makubwa kwa miaka minane mfululizo na kufika mapato ya Sh 640 bilioni.

Akizungumza wakati wa kikao kazi cha MSD na wahariri na waandishi wa habari Jijini Dodoma, Mfamasia kutoka kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini, Lilian Magesa amesema katika kipindi cha miaka minne mapato ya MSD yameongezeka kwa asilimia 103 kutoka Sh315.12 bilioni hadi kufikia Sh 640,5 bilioni mwaka 2024/25.

“Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa upatikanaji wa bidhaa za afya Kwa washitiri kutoka asilimia 42 mwaka 2021/22 hadi asilimia 73 Machi, 2026.

Amesema mafanikio mengine ni kuongezeka kwa mizunguko ya usambazaji wa bidhaa za afya kwenda vituo vya kutolea huduma za afya kutoka mizunguko minne kwenda mizunguko sita kwa mwaka huku ununuzi wa bidhaa za kuwezesha uzazi pingamizi ( CEmONO) umefikia asilimia 100.

Ameongeza kuwa mafanikio mengine mashine 162 za kusafisha damu(dialysis) zimesambazwa kutoka mashine 60 mwaka 2021/2022 zilizogharimu Sh 10.14 bilioni.

Pia kukamilisha ujenzi wa maghala ya kisasa yanayokidhi viwango vya uhifadhi na kuanza kutumika katika Kanda ya Dodoma na Mtwara -mita za mraba 12,000.Aidha kuanza kwa ujenzi wa ghala la Chato mkoani Geita lilifikia asilimia 42 ya utekelezaji.

Mafanikio mengine ni uanzishwaji wa kampuni tanzu ijulikanayo kama MSD Medipharm Manufacturing Company yenye jukumu la kusimamia uzalishaji unaotekelezwa kibiqshara, kiwanda cha mipira ya mikono -Idofi na ongezeko la thamania bidhaa zinazonunuliwa kutoka kwa wazalishaji wa ndani kutoka Sh15.90 bilioni zilizonunuliwa mwaka 2021/22 hadi Sh98.72 bilioni mwaka 20/2024/25, ”amesema.

*Imeandaliwa na Caen-Tausi Mbowe

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *