KIUNGO wa Simba, Neo maema amefunguka kwamba kuna raha yake kucheza mchezo mkubwa wa Dabi ya Kariakoo ikiwa na tofauti kubwa na dabi zingine kubwa ambazo amewahi kucheza.

Akizungumza na Mwanaspoti, Maema ambaye ameanza kuonyesha moto wake, amesema amecheza dabi nyingi ikiwemo zile za nchini kwao Afrika Kusini akiwa na Mamelodi Sundown.

Maema amesema Dabi ya Kariakoo ni tofauti na presha ya kwanza inaanzia nje kwa mashabiki ambao kila mmoja anataka kuona timu anayoshabikia inashinda kisha kuhamia uwanjani.

Kiungo huyo amesema kwao Afrika Kusini ni tofauti na presha ya mechi hiyo  kubwa inakuwa uwanjani ingawa mashabiki hujaa viwanjani lakini hawana mivutano kuelekea mechi hiyo.

MAE 01

“Nimeona na kucheza dabi nyingi lakini hii ya Tanzania ina utofauti mkubwa, kule Afrika Kusini presha inakuwa kwa timu tu ndani ya uwanja lakini hapa nimeona tofauti presha inaanzia nje kwa mashabiki kwanza,” amesema Maema.

“Mashabiki hapa wana kiu ya kuona timu zao zinashinda watafanya kila kitu kuhusu timu zao kushinda na bado watakuja uwanjani kuhakikisha wanawashangilia ili mtimize malengo.”

Aidha Maema ameongeza kuwa, ana kiu ya kuona Simba inashinda dabi ya kwanza tangu atue Tanzania akijivunia kikosi chao ambacho kinaundwa na wachezaji wenye njaa ya matokeo.

“Natamani kuona tunashinda dabi ya kwanza nikiwa hapa Simba, tulishindwa kufanya hivyo kwenye mechi mbili zilizopita msimu huu lakini kwa sasa ukiangalia kikosi chetu kimeimarika sana kina wachezaji wenye njaa sana ya mafanikio.

MAE 02

“Ukiangalia kule mbele kuna washambuliaji wanaofanya vizuri lakini kwenye kiungo nako kuna watu bora ambao wanajua kuchezesha timu na ile safu ya ulinzi nayo imeendelea kufanya vizuri.

“Naamini mashabiki wetu watakuja kwa idadi kubwa tena kutupa nguvu, huwa inatia nguvu unapoona uwanja umepambwa na mashabiki wa timu yako, siku zote wamekuwa wakifanya hivyo,” amesema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *