
Baada ya ziara yake nchini Oman na kuzungumza kwa simu na mwenzake wa Uturuki, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amerudi Islamabad Jumapili, Aprili 26. Asubuhi ya Jumatatu, Aprili 27, Waziri wa Mambo ya Nje amewasili Saint Petersburg, Urusi; anatarajia kukutana kwa mazungumo na rais Vladimir Putin.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amewasili leo Jumatatu Saint Petersburg, Urusi, ambapo atakutana na Vladimir Putin, hatua ya hivi karibuni katika safari ya kidiplomasia kuhusu vita katika Mashariki ya Kati, baada ya mkutano ulioshindwa na Marekani huko Islamabad.
“Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyed Abbas Araghchi amewasili Saint Petersburg, Urusi, Jumatatu asubuhi kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin,” vyombo kadhaa vya habari vya serikali ya Iran vimeripoti.
Akiwa Pakistan, Araghchi alikutana na viongozi kadhaa wakuu, akiwemo Mkuu wa Jeshi la Pakistan, Jenerali Asim Munir, Waziri Mkuu Shehbaz Sharif, na Waziri wa Mambo ya Nje Ishaq Dar. Baada ya mazungumzo hayo, alielekea Oman kwa mashauriano zaidi kabla ya kurejea tena Islamabad kwa mazungumzo ya ziada na wapatanishi wa eneo hilo.
Hata hivyo, juhudi za kuanzisha tena mazungumzo kati ya Tehran na Washington zilipata pigo mnamo siku ya Jumamosi baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kufuta safari ya wajumbe wake, Steve Witkoff na Jared Kushner, waliotarajiwa kwenda Islamabad kwa mazungumzo hayo.
Trump alieleza kupitia Fox News kwamba ikiwa kweli Iran inataka mazungumzo, “wanaweza kuja kwetu, au wanaweza kutupigia simu,” akisisitiza kuwa Marekani haitashiriki mazungumzo yasiyo na tija.