
Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kuendelea kufungwa kwa Benki katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa M23/AFC katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini, kumesababisha changamoto kubwa ya kibinadamu kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Mpango wa chakula duniani WFP.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hatua ya kufungwa kwa Benki, ilichukuliwa na serikali na Kinshasa baada ya waasi hao kuudhibiti mji wa Goma, lengo likiwa ni kulinda fedha za wateja na kuzuia M23/AFC kutumia Benki hizo kwa shughuli zake.
Hata hivyo, ripoti ya WFP inasema hatua hiyo imeathiri pakubwa upatikaji wa fedha za msaada ambayo mikoa ya Kivu Kusini na Kaskazini, ilistahili kupkea Dola za Marekani Milioni 75, lakini mpaka sasa ni Dola Milioni 39 ndizo zilizopatikana.
WFP inasema, msaada sio tu chakula lakini pia fedha, zinazopatikana ili kuwapa waathiriwa wa vita kununua wanachotaka.
Aidha, Shirika hilo linasema bila Benki, mfumo mzima wa kuwezesha utoaji wa msaada, umeathirika pakubwa kupitia mpango wake wa “Chakula Sokoni,” ambapo wenye mahitaji hupewa pesa ili kwenda kujinunulia chakula sokoni.
WFP inasema mpango huo, ulikuwa unawasaidia maelfu ya wahitaji,,a asilimia 83 walikuwa wameridhika ambapo biashara zilikuwa zinaimarika kwa sababu ya mzunguko wa fedha, lakini kwa sababu huduma za Benki zimesitishwa msaada huo wa kutoa fedha umetatizika.