
Mamlaka za baharini zinaonya kuhusu tishio kubwa kwa meli zilizoko pwani ya Somalia, baada ya mwishoni mwa juma lililopita, maharamia wa kisomali kuiteka meli moja ya mizigo kwenye ghuba ya Mareeyo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shirika la operesheni za Biashara ya Baharini la Uingereza, UKMTO, kwenye taarifa yake, limesema tukio hili lilitokea siku ya Jumapili wakati watu wenye silaha waliabiri meli hiyo takribani maili sita kutoka Garacad na kuielekeza kwenye eneo la maji ya Somalia.
Wiki iliyopita takriban meli nne zililengwa, ikiwa ni pamoja na meli ya uvuvi, lori la mafuta, na meli nyingine za kibiashara.
Uharamia katika eneo hilo ulikuwa umepungua kwa kiasi kikubwa katika muongo mmoja uliopita, kufuatia doria za kimataifa za wanamaji na kuboreshwa kwa hatua za usalama za ndani, matukio ya hivi karibuni yakiashiria kufufuka kwa uharamia, unaoweza kuvuruga tena njia kuu za biashara za kimataifa.
Katika kilele cha uharamia kati ya mwaka 2005 na 2012, mashambulizi katika Pembe ya Afrika yalizalisha mamia ya mamilioni ya dola katika malipo ya fidia, kulingana na makadirio ya Benki ya Dunia.