#HABARI: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amewasili mkoani Kigoma kwa ziara ya siku mbili ambapo kesho, Aprili 30, 2026, anatarajiwa kuifunga rasmi kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo.
Hatua hiyo inajumuisha makabidhiano ya miundombinu ya kudumu na vitendea kazi kwa Serikali kwa ajili ya matumizi mengine, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya pande tatu kati ya Tanzania, Burundi, na Shirika la UNHCR ya kuhimiza urejeshaji wa wakimbizi nchini kwao kwa hiari.
Kufungwa kwa kambi hiyo kunafuatia ombi la Serikali ya Burundi kuongeza muda wa utekelezaji hadi mwisho wa mwezi huu, huku mpango huo ukiainisha kuwa wakimbizi waliopo Nyarugusu wanatarajiwa kurejea kwao ifikapo Juni 30, 2026.
Serikali imetaja hatua hii kama mafanikio makubwa katika kudhibiti changamoto mbalimbali zinazotokana na uwepo wa wakimbizi, huku ikisisitiza dhamira ya kuimarisha usalama na kurejesha mazingira ya kambi hizo katika matumizi ya kimaendeleo kwa wananchi wa maeneo husika.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)