Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya ndani Jacquemain Shabani ameponea kura ya kukosa imani naye bungeni kufuatia mvutano wa uhalali wa saini zilizokusanywa kumtaka aondoke madarakani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mswada huo uliogongwa mwamba bungeni siku ya Jumatano, uliwasilishwa na mbunge Yangotikala Senga.

Hata hivyo, mswada huo haukuenda mbali baada ya wabunge kusema mbunge huyo hakufuata utaratibu wa kuuwalisha, na saini zilizokuwa zimekusanywa hazikupatikana kwa njia halali.

Kutokana na mapungufu hayo, Spika wa bunge aliamua kuwa, hakukuwa na haja ya kujadili au kuupigia mswada huo, baada ya mbunge Gary Sakata kutoa hoja za kuridhisha kwa kuonesha kuwa mswada huo haukuwaslishwa kwa utaratibu  na kwa mujibu wa kanuni za bunge.

Hata hivyo, mbunge Yangotikala kutoka Kisangani aliyewasilishwa mswada huo, aliwaeleza wabunge kuwa, Naibu Waziri Mkuu Jacquemain Shabani anapaswa kuondoka kwenye nafasi hiyo kwa kushindwa, kuhakikisha kuwa kuna usalama, katika majimbo mbalimbali nchini DRC hasa yale ya Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *