Wakimbizi wa ndani waliorejea makaazi yao wilayani Rutshuru Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuanza kurejea kwa amani katika eneo lao, sasa wapo kwenye hatari kubwa ya kukabiliwa na baa la njaa, baada ya mazao yao kuvamiwa na viwavi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mahindi na maharagwe katika Wilaya ya Rutshuru yameharibiwa kwa asilimia kubwa na viwavi.

Wakulima wamepoteza matumaini  ya kupata mavuno mazuri na kwamba watakosa kupata mbegu ya kutumia katika siku zijazo.

Wakulima sasa wanahofu ya kukabiliwa na baa la njaa.

“Shida tunazokabiliwa nazo hapa shambani, wadudu hawa wanatuhangaisha sana wanakula mahindi, maharagwe hatujui tufanye nini kwa Sasa,tunateseka sana ,Hali hii ilianza mwezi huu wa Aprili . Siku zijazo hali hii itasababisha njaa kwa sababu wadudu hawa wameharibu mimea kabisa.” Alisema mmoja wa Wakulima.

Marc Banura, mtaalamu wa kilimo wa kujitegemea Wilayani Rutshuru anawataka wakulima kuheshimu kikamilifu kalenda ya mazao ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

“Watu walime mapema. Unaona baadhi ya mashamba yanayovamiwa na viwavi, ni yale ambayo yamelimwa hivi karibuni bila ya kuheshimu kalenda ya kilimo.” Alisema Marc Banura mtaalam wa kilimo.

Hali hii inaendelea kuwatia wakulima na wakazi katika eneo hili hofu na kutokea kwa njaa katika eneo nzima la mashariki ya Congo.

TSCHUBE NGOROMBI GOMA RFI KISWAHILI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *