Katika barua kwa Bunge la Marekani, Rais Donald Trump ameandika kwamba vita dhidi ya Iran “vimekwisha,” akizingatia sheria ya Marekani inayoweka kikomo cha mzozo bila idhini ya bunge hadi siku 60. Mapema Ijumaa, alisema “hajaridhika” na pendekezo jipya lililotolewa na Iran mnamo Mei 1 kujaribu kuahirisha mazungumzo. 

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Mareani Donald Trump alisema siku ya Ijumaa kwamba vita dhidi ya Iran “vimekwisha” katika barua iliyotumwa kwa wabunge, hivyo akidai kwamba alikuwa akifuata sheria inayomtaka rais wa Marekani kupata idhini ya bunge ili kuongeza mzozo zaidi ya siku 60.

“Mnamo Aprili 7, 2026, niliamuru kusitisha mapigano kwa wiki mbili. Tangu wakati huo, kusitisha mapigano kumeongezwa muda.” Hakujakuwa na ubadilishanaji wa risasi kati ya vikosi vya Marekani na Iran tangu Aprili 7, 2026. Vita vilivyoanza Februari 28, 2026, vimekwisha,” aliandika Donald Trump siku ya mwisho ya kupata idhini ya bunge ili kuendelea na vita dhidi ya Iran.

Je, mzozo huo umekwisha kweli? 

Kinadharia Donald Trump alikuwa na hadi Ijumaa, Mei 1, kuomba idhini kutoka kwa Bunge la Marekani ili kuendelea na vita. Lakini utawala wake ulipendekeza kwamba ungepuuza wajibu huu, kwani upinzani kutoka chama cha Democratic ulijikuta hauna nguvu ya kuutekeleza.

Hata hivyo, rais wa Marekani alituma barua kwa maafisa wa bunge akiwaarifu kwamba vita dhidi ya Iran “vimekwisha,” ingawa wabunge kadhaa kutoka chama cah Democratic walisema kwamba uwepo wa vikosi vya Marekani katika eneo hilo unaonyesha vinginevyo.

Vita hivyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu, hasa nchini Iran na Lebanon, na Matokeo yake yanaendelea kutikisa uchumi wa dunia. Duru ya kwanza ya mazungumzo ya moja kwa moja huko Islamabad mnamo Aprili 11 hayakuzaa matunda na hadi sasa hayajaleta matokeo yoyote.

Mgogoro huo unaendelea kwa njia zingine: Washington imeweka vizuizi kwenye bandari za Iran kulipiza kisasi kwa kufungwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz na Tehran, ambapo sehemu ya tano ya hidrokaboni inayotumiwa duniani imekuwa ikipita hapo awali.

Serikali ya Marekani ilitangaza vikwazo vipya dhidi ya maslahi ya Iran siku ya Ijumaa na kuonya kwamba wale wanaolipa ushuru kwa mamlaka ya Tehran ili kupitisha mlango-bahari huo watakabiliwa kali na adhabu ya Marekani.

Meli ya USS Gerald Ford, meli kubwa zaidi ya kubeba ndege duniani, imeondoka Mashariki ya Kati, lakini meli 20 za Jeshi la Wanamaji la Marekani, ikiwa ni pamoja na meli nyingine mbili za kubeba ndege, bado ziko katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *