
Mkuu wa Shirikisho la Soka la Palestina amekataa ombi la rais wa FIFA, Gianni Infantino la kupiga picha na mwakilishi wa utawala haramu wa Israel.
Gianni Infantino alijaribu kumuweka rais wa Shirikisho la Soka la Palestina, Jibril Rajoub pamoja na mwakilishi wa shirikisho la mpira wa miguu la utawala ghasibu wa Israel kwa ajili ya kupiga picha katika Mkutano wa 76 wa FIFA uliofanyika Canada, lakini upande wa Palestina ulikataa suala hilo.
Jibril Rajoub alifoka jukwaani akisema: “Tuko kwenye mateso” na baadea ya hapo aliondoka eneo hilo mara moja.
Suzanne Shalabi, naibu mkuu wa Shirikisho la Soka la Palestina, ameiambia Reuters kwamba Rajoub alisema: “Siwezi kupeana mikono na mtu ambaye Waisraeli wamemleta ili kutakasa uhalifu wao wa kifashisti na mauaji ya kimbari.”
Hapo awali, katika hotuba yake, Jibril Rajoub alikuwa ameitaka tena FIFA kukabiliiana na shughuli za vilabu vya Israel katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vya Ukingo wa Magharibi na akizitaja kuwa ni kinyume cha sheria.