Mjumbe wa Idara ya Siasa ya Hamas, Mohammed Nazzal, amesema kuwa ombi la kukabidhiwa silaha za harakati hiyo ni kisingizio kinachotumiwa na utawala wa Kizayuni wa Israel ili kukwepa utekelezaji wa majukumu yake.

Nazzal ameeleza kuwa lengo la utawala wa Kizayuni ni kuyapokonya silaha makundi yote ya mapambano ya ukombozi, na sharti hilo limetumiwa na Benjamin Netanyahu kama kisingizio cha kuchelewesha utekelezaji wa majukumu ya utawala wa kizayuni katika hatua ya kwanza ya makubaliano ya kusitishwa mapigano.

Kiongozi wa Hamas ameashiria uzoefu wa huko nyuma ambapo Hamas na makundi mengine ya mapambano yalijitolea vya kutosha, ikiwa ni pamoja na kukabidhi mateka waliokuwa hai na waliokufa wa Israel, lakini wavamizi waliendelea kushambulia na kuua watu wa Ukanda wa Gaza.

Nazzal amesisitiza kuwa: Hamas inataka mpango wazi wa uendeshaji, muda maalumu, na dhamana za pande zote mbili ili kuhakikisha kwamba vita na mauaji ya halaiki havirudi. Ametaja vitisho vya Netanyahu vya kuanzisha tena vita kuwa ni “usaliti usio na maana.”

Ameongeza kuwa msimamo wa Hamas hauchochewi na maslahi ya kichama au ya ubinafsi, bali unatokana na maslahi ya watu wa Palestina, ambao wanataka dhamana halisi ya kukomeshwa mauaji ya kimbari, kuhakikisha kwamba hayatokei tena, na kupata haki zao halali za kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *