Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa kauli rasmi kufuatia ripoti ya Tume ya Uchunguzi ßiliyoundwa kuchunguza matukio ya ghasia yaliyotokea Oktoba 29, 2025, kikisisitiza kulinda umoja wa kitaifa na mustakabali wa nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mei 4, 2026 jijini Dodoma, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, amesema chama hicho kimeipokea ripoti kwa uzito, kikitambua mchango wake katika kulinda mshikamano wa Taifa na kujenga msingi imara kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

“Tume imefanya kazi kwa uhuru, weledi na uzalendo wa hali ya juu. Pongezi maalum kwa Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Othman Chande, pamoja na wajumbe wote waliotekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa.

CCM pia imewashukuru Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kutoa maoni na ushahidi wao kwa utulivu na ushirikiano mkubwa wakati wa zoezi la ukusanyaji wa taarifa, jambo lililosaidia kukamilika kwa kazi ya tume hiyo kwa mafanikio.

Kuhusu mapendekezo yaliyotolewa, CCM imeeleza kuyaunga mkono kikamilifu na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuyapokea na kuonesha utayari wa kuyafanyia kazi kwa manufaa ya t
Taifa.

Hata hivyo, chama hicho kimesisitiza kuwa njia sahihi ya kufikia suluhu ya kudumu ni kupitia maridhiano ya kitaifa, sambamba na kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo halisi cha ghasia hizo, waliohusika, malengo yao na hatua stahiki za kuwawajibisha wahusika.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *