
Siku mbili baada ya mahojiano marefu na waandishi wa habari wa Senegal, ambapo Rais alisisitiza mamlaka yake ya kumfukuza Waziri Mkuu wake iwapo atapoteza imani naye na kushughulikia hoja zake za kutokubaliana na chama tawala cha African Patriots of Senegal for Work, Ethics, and Fraternity (PASTEF), Bassirou Diomaye Faye amemfuta kazi msemaji wa ikulu ya rais Ousseynou Ly, mwanaharakati wa muda mrefu wa PASTEF, akimbadilisha na Abdoulaye Tine, wakili na mratibu wa muungano wa Diomaye Rais.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff
Kwenye mitandao ya kijamii, majibu kutoka kwa wanaharakati wa PASTEF yalikuwa ya haraka, baadhi ya walishtuka kumuona Ousseynou Ly, mfuasi mwaminifu tangu mwanzo, akifukuzwa kazi. Ly alikuwa amesimama pamoja na Bassirou Diomaye Faye na Ousmane Sonko walipoachiliwa kutoka gerezani mnamo Machi 2024, wakati wa mkutano wao wa kwanza na waandishi wa habari.
“Hatua ya watu kufukuzwa serikalini inaanza,” amesema mwanaharakati mmoja, huku wengine wakizungumzia rais kuanza kuchukuwa hatua kwa “upendeleo wa wafuasi wake”. Huu pia ni uchambuzi wa Alioune Tine, mwanaharakati wa haki za binadamu na mttezi wa Ousmane Sonko kuwania katika nafasi ya rais mwaka wa 2024, ambaye anaona katika kufukuzwa huku “kitendo cha kwanza cha kutengana kwa kitaasisi” kati ya wakuu hao wawili serikalini: “Diomaye moy Sonko,” “Diomaye, ni Sonko” kwa Kiwolof, kauli mbiu hii ya kampeni ya urais “imepotea” anasema Alioune Tine.
Anajiandaa “kwa vita vya kisiasa” vinavyomsubiri
Alioune Tine anaona kufukuzwa huku kwa msemaji wa ikulu ya rais kama matokeo ya moja kwa moja ya kauli za Mkuu wa Nchi siku ya Jumamosi: yaani, kwamba ndiye mwenye mamlaka ya kumteua au kumfukuza mtu yeyote serikalini.
Kwa kumteua Abdoulaye Tine, wakili asiye na uhusiano wowote na PASTEF, kama msemaji mpya waikulu ya rais—Tine mwenyewe akiwa mkuu wa chama kidogo ndani ya muungano wa Diomaye Rais—mkuu wa nchi anakusanya wafuasi wake, kulingana na mwandishi wa habari na mchambuzi Assane Samb, kana kwamba anajiandaa vyema kwa vita vya kisiasa vinavyomsubiri.
Mnamo Mei 4, Waziri Mkuu alitangaza kwamba angezungumza hivi karibuni ili kutathmini miaka yake miwili madarakani na, baada ya muda, alitahadharishwa.
Akiwa amealikwa kuzungumza kwa simu wakati wa mkutano wa tawi la vijana la chama cha PASTEF, kiongozi wa chama hicho, Ousmane Sonko, alisifu mabadiliko ya chama chake cha kisiasa: “chama cha kutafakari, cha kutoa maoni,” “chama chenye programu,” alisema. “Chama hiki ni chenu,” Waziri Mkuu aliwahakikishia, kabla ya kuwaonya vijana wa PASTEF dhidi ya kugombea nafasi. “Kugombea huku kwa nafasi, mimi, mimi, mimi,” Ousmane Sonko alidai, “msijihusishe na hilo,” Waziri Mkuu aliongeza huku akipigiwa makofi makubwa.
Kauli hii ilionekana kama jibu la moja kwa moja kwa Mkuu wa Nchi, Bassirou Diomaye Faye, ambaye siku iliyopita alikuwa ametumia muda mwingi akielezea hadharani, kwa mara ya kwanza, jukumu kuu alilofanya katika uundaji wa PASTEF. Kauli mbiu “kujitolea kwa ajili ya taifa” ilitoka kwangu, alielezea, kwa mfano, katika uthibitisho usio wa kawaida wa nguvu zake ndani ya chama na kwa mkuu wa nchi.
“Ni jibu la kulipiza kisasi,” anasema mchambuzi wa masuala ya kisiasa. Na anabainisha kile kinachoonekana kuwa tabia nchini Senegal: kauli ya rais inafuatwa kimfumo na kauli kutoka kwa waziri mkuu…