
Wakati meli mbili zikikamatwa na nyingine kushambuliwa mwezi Aprili pwani ya Somalia, meli ya Eureka, yenye bendera ya Togo, ilitekwa nyara na watu wenye silaha waliokuwa wakisafiri kwenye meli za mwendo kasi Jumamosi, Mei 2. Jambo hili linaaminika kuhusishwa kwa kiasi kikubwa na kuzingirwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz, kitovu cha mzozo kati ya Iran, Israel, na Marekani.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Manahodha wa meli za mizigo na meli za mafuta wanahimizwa kuwa macho zaidi katika njia hii yenye shughuli nyingi ya meli: kwani meli nyingi zinalazimika kusafiri kuzunguka Somalia ili kuepuka Mlango-Bahari wa Hormuz, kitovu cha mzozo wa sasa kati ya Iran upande mmoja, na Marekani na Israel upande mwingine, vitendo vya uharamia vinaongezeka tena katika eneo hilo.
Watu wenye silaha wakiwa kwenye meli za mwendo kasi wanaweza kushambulia meli na kuwachukua wafanyakazi wao mateka huku wakisubiri fidia. Kwa mfano, siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita, Mei 2, meli ya mafuta ya Eureka, iliyokuwa ikisafiri chini ya bendera ya Togo, ilitekwa nyara kutoka pwani ya Yemen kabla ya kuelekezwa kwenye pwani ya Somalia.
Kabla ya hapo, meli mbili zilikamatwa na nyingine kushambuliwa mwezi Aprili. Ingawa, kulingana na Omar Mahmood, mchambuzi katika shirika linalohusika na kutatua migogoro la International Crisis group (ICG), mitandao hii ya uhalifu wa uharamia haijawahi kutoweka kabisa, kuibuka tena kwa mashambulizi yao katika wiki za hivi karibuni ni matokeo ya fursa wanayokusudia kutumia.
“Nadhani jambo hili ni sehemu ya muktadha mpana unaohusishwa na hali ya kijiografia ya kimataifa.” Kuzingirwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz na vita na Iran vimehamisha sehemu kubwa ya umakini wa baharini hadi eneo hili, kaskazini kidogo, na maharamia wa Somalia wanakusudia kutumia fursa hii,” anaelezea, kabla ya kuendelea: “Mwishoni mwa mwaka 2023 na mwanzoni mwa mwaka 2024, tayari tumeona ongezeko jipya la uharamia katika eneo hilo, kisha mambo yakatulia kidogo mwanzoni mwa mwaka 2025, huku kukiwa na matukio machache tu yenye madhara madogo.”
Ili kukabiliana na maharamia hawa wanaojipanga kwa makabila katika eneo la Puntland kaskazini mwa Somalia, mamlaka ya nchi hiyo ina uwezo mdogo, hasa kwa vile tayari wamehamasishwa dhidi ya wapiganaji wa kijihadi wa kundi la Al Shabab na Islamic State ambao pia wanaendesha harakati zao katika eneo hilo.
Baada ya kukithiri mwaka wa 2011, vitendo vya uharamia pwani ya Somalia vilipungua sana kutokana na kupelekwa kwa vikosi vya kimataifa vya majini na kuimarishwa kwa hatua za usalama wa baharini.