Marekani. Mwanamke bilionea kutoka India, Sudha Reddy, alivutia macho ya wengi kwenye Met Gala 2026 baada ya kuingia kwenye zulia jekundu akiwa amevaa mkufu wa Tanzanite wenye thamani ya dola milioni 15 uliotoka Tanzania.

Kito hicho cha kipekee, kilikuwa na pendenti ya Tanzanite yenye rangi ya zambarau na bluu inayojulikana kama “Queen of Mererani,” iliyochimbwa kutoka Milima ya Mererani nchini Tanzania.

Jiwe hilo adimu liliwekwa katika cheni iliyopambwa kwa almasi katika mtindo wa rose. Jambo ambalo limezua mjadala katika usiku huo na kufanya mkufu huo kuzungumziwa na watu mbalimbali.

Reddy alivalia mkufu huo pamoja na gauni maalum lililobuniwa na mbunifu wa mavazi wa India, Manish Malhotra, likiwa limenogeshwa na ufundi wa kitamaduni wa India na urithi wa kitamaduni wa Hyderabad.

Vazi halo liliendana na kaulimbiu ya Met Gala 2026, ambayo ilichunguza uhusiano kati ya mitindo na sanaa.

Bilionea huyo, anayejulikana kwa kuonyesha vito adimu katika majukwaa ya kimataifa, alikamilisha muonekano wake kwa kuongeza vito vingine, ikiwa ni pamoja na pete za zumaridi na almasi.

Muonekano wa Sudha Reddy ulikuwa wa kipekee sana kwenye Met Gala, kiasi kwamba alijitofautisha na mastaa wengine wote waliokuwepo.

Alionekana kama mtu anayejua kuchanganya vitu vitatu muhimu katika mitindo yake.  Urithi na utamaduni wake. Hii inamaanisha kuwa mavazi na vito vyake havikuwa vya urembo tu, bali vilibeba ujumbe na historia nyuma yake.

Kwa upande mwingine, mkufu wake wa Tanzanite uliokuwa wa thamani kubwa ulisaidia sana kuitangaza Tanzania duniani. Kwa kuwa alivaa jiwe hilo kwenye tukio kubwa la kimataifa la mitindo, watu wengi waliliona na kulizungumza. Hivyo kuongeza umaarufu wa Tanzanite, hii ilifanya jiwe hilo adimu lijulikane zaidi na kuonyesha thamani yake kwenye jukwaa kubwa la dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *