
Miezi miwili baada ya kuanza kwa mgogoro katika Mashariki ya Kati, Mlango-Bahari wa Hormuz, njia muhimu kwa biashara ya kimataifa, bado imefungwa na Iran. Hili ni pigo kubwa kwa uchumi wa Ghuba unaosafirisha mafuta na gesi yao kwenda sehemu nyingine za dunia. Mlango-Bahari wa Hormuz pia ni lango la bidhaa. Na ili kuendelea kufanya usafirishaji, nchi za Ghuba zimetafuta njia mbadala.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ili kuipita Mlango-Bahari wa Hormuz, uliozuiwa tangu mwanzoni mwa mwezi Machi na vita katika Mashariki ya Kati, makampuni ya meli yalibadilisha njia zao haraka. Baadhi ya meli za mizigo sasa zinaelekea kwenye bandari ndogo zilizopo ndani ya mlango wa mlango-bahari.
Katika Falme za Kiarabu, bandari ya Khor Fakkan imjikuta shughuli zake zikiongezeka. Kila siku, zaidi ya malori 6,000 yanahitajika kupakua makontena, ikilinganishwa na takriban malori mia moja kabla ya vita. Lakini bandari hii sasa inajikuta haina tena na fasi ya kupokea makontena hayo, na foleni ya malori inazidi kuwa ndefu.
Bandari ya Jeddah, lango la kuingia Bahari Nyekundu
Upande mwingine wa Rasi ya Arabia, kwenye Bahari Nyekundu, bandari ya Jeddah nchini Saudi Arabia imekuwa njia mbadala kuu. Meli kubwa zinazotumika kupakia makontena zinazowasili kutoka Mfereji wa Suez hupakua mizigo yao huko, ambayo husafirishwa kwa barabara kuvuka jangwa hadi Falme za Kiarabu, Bahrain, au Kuwait. Matokeo yake, bandari hiyo inashughulikia kontena 120,000 kila wiki, ikilinganishwa na 50,000 kabla ya vita.
Uthibitisho wa nia mpya katika njia hii, Meli kubwa ya MSC itazindua huduma mpya wiki ijayo kati ya Ulaya na Rasi ya Arabia, kupitia Mfereji wa Suez. Hatimaye, mgogoro katika Mashariki ya Kati umerudisha miradi mingine katika uangalizi, kama vile ukanda wa IMEC, uliozinduliwa mwaka wa 2023. Njia hii inalenga kuunganisha India na Ulaya kupitia Mashariki ya Kati, ikipita kwa kiasi fulani Mlango-Bahari wa Hormuz. Lakini ili njia mbadala hii ionekane, inahitaji uhusiano kati ya Saudi Arabia na Israel, ambao sasa hauna uhakika zaidi kuliko hapo awali.