Mbunge wa Jimbo la Msalala,Mhe. Mabula Magangila ameiomba Wizara ya Maji kushughulikia changamoto ya gharama kubwa za kuunganisha huduma ya maji majumbani katika maeneo ya vijijini akisema hali hiyo bado inawanyima wananchi lengo halisi la huduma ya maji safi na salama.

Akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2026/27, Mhe. Magangila amemwelekeza Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso, kufuatilia kwa karibu suala hilo na kuhakikisha kunakuwa na mkakati wa miradi midogo midogo itakayosaidia kusogeza huduma ya maji karibu zaidi na wananchi.

Amesema licha ya uwepo wa miradi mikubwa ya kusambaza maji vijijini bado gharama za kuvuta maji hadi kwenye kaya ni kubwa jambo linalowalazimu wananchi wengi kuendelea kutumia maji ya vituo vya pamoja badala ya kuyapata majumbani mwao.

“Miradi yetu mingi inalenga kufikisha maji kijijini, lakini gharama za kuvuta maji majumbani bado ni kubwa sana. Niombe wizara itekeleze miradi midogo midogo ya kusogeza maji karibu na wananchi ili gharama ya kuunganisha maji ipungue. Hapo ndipo tutakapokuwa tumemtua mama ndoo kichwani—badala ya kuchota maji kwenye vituo vya pamoja, tunataka wananchi wetu wachote maji majumbani kwao,” amesema Magangila.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *